2 Wafalme 2:10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
10 Elia akajibu: “Ombi lako ni gumu. Hata hivyo, ikiwa utaniona wakati nitakapoondolewa kwako, itafanyika vile kwako. Lakini usiponiona, basi haitafanyika vile.”
Elisha alipoona tukio hilo, akalia: “Baba yangu, baba yangu! Ulikuwa wa lazima kuliko magari ya Israeli na wapanda-farasi wake!” Basi, Elisha hakumwona tena Elia. Halafu Elisha akashika nguo zake na kuzipasua vipande viwili.