Tangu wakati ule nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza waadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa mwenye utukufu kama wakubwa wengine katika dunia.
Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa mutindo wa wimbo “Ushuhuda wa mayungiyungi.” Mashairi ya Daudi ya kufundisha yanayoelekea wakati alipopigana na Wasuria katika Mesopotamia na Zoba naye Yoabu aliporudi nyuma na kuwaua Waedomu elfu kumi na mbili katika bonde la Chumvi.