Wakaomboleza, wakalia na kufunga kula mpaka magaribi kwa ajili ya Saulo, Yonatani mwana wake, na inchi ya Waisraeli, watu wa Yawe, kwa maana wengi kati yao waliuawa katika vita.
Daudi akawaamuru vijana wake, nao wakawaua. Wakawakata mikono na miguu. Halafu wakawatundika juu ya muti pembeni ya kisima kule Hebroni. Lakini walikichukua kichwa cha Isiboseti na kukizika katika kaburi la Abeneri kule Hebroni.