2 Samweli 3:27 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200227 Abeneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimupeleka pembeni kwenye mulango sawa vile anataka kuzungumuza naye kwa siri. Hapo Yoabu akamukata Abeneri katika tumbo kwa sababu Abeneri alikuwa amemwua ndugu yake Asaeli, na Abeneri akakufa. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Mungu atamwazibu Yoabu kwa mauaji hayo aliyoyafanya bila baba yangu kuwa na habari. Yeye aliwaua watu wawili ambao walikuwa wa maana zaidi kuliko yeye, tena walimupita kwa wema; aliwaua Abeneri mwana wa Neri, jemadari wa kundi la waaskari Waisraeli, na Amasa mwana wa Yeteri, jemadari wa waaskari wa Yuda.
“Zaidi ya hayo, unajua vilevile yale Yoabu mwana wa Zeruya aliyonitendea, jinsi alivyowatendea majemadari wawili wa waaskari wa Israeli, Abeneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yeteri. Aliwaua wakati wa amani akitaka kulipiza kisasi kwa mauaji waliyofanya wakati wa vita. Aliwaua watu wasiokuwa na kosa, nami nikabeba lazima ya kifo cha watu wale kwa ajili ya vitendo vyake.