akisema: “Tendo kama hili lipite mbali nami; siwezi kulifanya mbele ya Mungu wangu. Basi ninaweza kunywa damu ya maisha ya watu hawa? Maana kwa kuyahatarisha maisha yao walileta maji haya.” Kwa hiyo Daudi hakukunywa maji yale. Hayo ndiyo mambo waliyotenda wale mashujaa watatu.