Waamoni walipoona kwamba Waaramu wamekimbia, nao vilevile walimukimbia Abisayi na kuingia katika muji. Yoabu akaacha kupigana na Waamoni, akarudi Yerusalema.
Tangu wakati ule nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza waadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa mwenye utukufu kama wakubwa wengine katika dunia.