16 Yawe alipovikaripia, pumzi ya pua yake ilifunua vilindi vya bahari na misingi ya dunia ikaonekana.
Moshi ulifuka kutoka katika pua yake, moto wenye kuteketeza ukatoka katika kinywa chake, makaa ya moto yakatokea.
na kuiambia: “Mwisho wako ni hapa, si zaidi! Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!”
Alikaripia bahari Nyekundu, ikakauka; akawapitisha humo kama katika inchi kavu.
Mashairi ya Asafu. Kwa nini, ee Mungu, umetutupilia kabisa? Mbona hasira yako inawaka juu ya kondoo wako?
Musikilize mashitaki ya Yawe, enyi milima, musikilize enyi misingi imara ya dunia! Yawe yuko na maneno juu ya watu wake. Yeye atatoa mashitaki juu ya Waisraeli.
Anaikaripia bahari na kuikausha, yeye anaikausha mito yote. Mbuga za Basani na mulima Karmeli zinanyauka, maua ya Lebanoni yanakauka.