Wakati ule, Abusaloma alikuwa amemuweka Amasa kuwa jemadari wa waaskari pahali pa Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Itira, Mwisimaeli. Mama yake aliitwa Abigaili binti wa Nahasi, aliyekuwa dada ya Zeruya mama ya Yoabu.
Muulize vilevile Amasa kama yeye si damu yangu. Tena Mungu aniue ikiwa simufanyi yeye kuwa jemadari wa kundi langu la waaskari tangu leo pahali pa Yoabu.’ ”