25 Sewa alikuwa katibu. Zadoki na Abiatari walikuwa makuhani.
Kuhani Abiatari akatoka, hata na kuhani Zadoki akatoka pamoja na Walawi wote wakilibeba Sanduku la Agano la Mungu. Wakaliweka lile Sanduku la Mungu chini, mpaka watu wote walipopita kutoka Yerusalema.
Ira wa muji Yairi alikuwa vilevile kuhani wa Daudi.
Zadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiatari walikuwa makuhani. Seraya alikuwa katibu.
Adonia akafanya shauri na Yoabu mwana wa Zeruya, na kuhani Abiatari. Nao wakamufuata na kumwunga mukono.
Lakini kuhani Zadoki, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Natani na Simei, na Rei pamoja na walinzi wa Daudi, hawakumwunga Adonia mukono.
Zadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiatari walikuwa makuhani; Sausa alikuwa katibu;