30 Yoabu aliporudi kutoka kumufuatilia Abeneri, aliwakusanya watu wake wote, akagundua kwamba watumishi kumi na tisa wa Daudi walikosekana, bila kuhesabu Asaeli.
Abeneri na watu wake walipita katika bonde la Araba usiku kucha. Wakavuka Yordani, wakatembea muchana wote mpaka Mahanaimu.
Lakini watumishi wa Daudi walikuwa wamewaua watu mia tatu makumi sita kutoka kabila la Benjamina pamoja na watu wa Abeneri.