Watu wote waliogandamizwa au waliokuwa na madeni au wale wenye huzuni walijiunga na Daudi. Jumla yao ilikuwa watu yapata mia ine, naye akakuwa kiongozi wao.
Kisha siku tatu, Daudi na watu wake wakarudi Ziklagi. Waamaleki walikuwa wamekwisha kushambulia Negebu pamoja na muji wa Ziklagi na kuuteketeza kwa moto.