2 Samweli 2:18 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200218 Wana watatu wa Zeruya, Yoabu, Abisayi na Asaeli walikuwa pale pale. Asaeli alikuwa na mbio kama paa. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
“Zaidi ya hayo, unajua vilevile yale Yoabu mwana wa Zeruya aliyonitendea, jinsi alivyowatendea majemadari wawili wa waaskari wa Israeli, Abeneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yeteri. Aliwaua wakati wa amani akitaka kulipiza kisasi kwa mauaji waliyofanya wakati wa vita. Aliwaua watu wasiokuwa na kosa, nami nikabeba lazima ya kifo cha watu wale kwa ajili ya vitendo vyake.
Hawa ndio waaskari shujaa wa Daudi: Asaheli ndugu ya Yoabu, Elihanani mwana wa Dodo, wa Betelehemu, Samoti wa Harodi, Helesi wa Peloni, Ira mwana wa Ikesi wa Tekoa, Abiezeri wa Anatoti, Sibekai wa Husa, Ilai wa Ahohi, Maharai wa Netofati, Heledu mwana wa Bana wa Netofati, Itai mwana wa Ribai, kutoka Gibea katika kabila la Benjamina, Benaya wa Piratoni, Hurai kutoka vijito vya Gasi, Abieli wa Araba, Azimaweti wa Baharumu, Eliaba wa Salaboni, wana wa Yaseni wa Gizoni, Yonatani mwana wa Sage wa Harari, Ahiyamu mwana wa Sakari wa Harari, Elifali mwana wa Uri, Heferi wa Mekerati, Ahiya wa Peloni, Hesero wa Karmeli, Naarai mwana wa Esibai, Yoeli ndugu ya Natani, Mibuhari mwana wa Hagiri, Zeleki wa Amoni, Naharai wa Beroti aliyekuwa mubebaji wa silaha wa Yoabu mwana wa Zeruya, Ira na Garebu, waliokuwa wa Itiri, Uria Muhiti, Zabadi mwana wa Alai, Adina mwana wa Siza wa kabila la Rubeni, mukubwa wa kabila la Rubeni, akiwa pamoja na watu makumi tatu, Hanani mwana wa Maka, Yosafati wa Miti, Usia wa Astera, Sama na Yeieli, wana wa Hotamu wa Aroeri, Yediaeli na ndugu yake Yoha, wana wa Simuri wa Tisi, Elieli wa Mahawi, Yeribali na Yosawia wana wa Elenama, Itima wa inchi ya Moabu, Elieli, Obedi, na Yasieli wa Mesoba.
Kutoka kabila la Gadi, hawa ndio waaskari mashujaa na walioelewa sana vita. Wakatoka kwao kwenda kujiunga na kundi la Daudi alipokuwa katika maficho kule katika jangwa. Walikuwa hodari wa kutumia mikuki na ngao, wenye nyuso za kuogopesha kama za simba, na katika milima walikuwa wepesi wa kukimbia kama swala. Kiongozi wao mukubwa alikuwa Ezeri. Alifuatwa na: Obadia, Eliabu, Misimana, Yeremia, Atai, Elieli, Yohana, Elisabadi, Yeremia, Makibanai.