2 Samweli 17:25 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200225 Wakati ule, Abusaloma alikuwa amemuweka Amasa kuwa jemadari wa waaskari pahali pa Yoabu. Amasa alikuwa mwana wa Itira, Mwisimaeli. Mama yake aliitwa Abigaili binti wa Nahasi, aliyekuwa dada ya Zeruya mama ya Yoabu. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Mungu atamwazibu Yoabu kwa mauaji hayo aliyoyafanya bila baba yangu kuwa na habari. Yeye aliwaua watu wawili ambao walikuwa wa maana zaidi kuliko yeye, tena walimupita kwa wema; aliwaua Abeneri mwana wa Neri, jemadari wa kundi la waaskari Waisraeli, na Amasa mwana wa Yeteri, jemadari wa waaskari wa Yuda.
“Zaidi ya hayo, unajua vilevile yale Yoabu mwana wa Zeruya aliyonitendea, jinsi alivyowatendea majemadari wawili wa waaskari wa Israeli, Abeneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yeteri. Aliwaua wakati wa amani akitaka kulipiza kisasi kwa mauaji waliyofanya wakati wa vita. Aliwaua watu wasiokuwa na kosa, nami nikabeba lazima ya kifo cha watu wale kwa ajili ya vitendo vyake.
Halafu Roho akamujaza Amasai, mukubwa wa wale watu makumi tatu, naye akasema: “Sisi ni watu wako, ee Daudi! Tuko upande wako, ee mwana wa Yese! Amani, amani ikuwe kwako, na amani ikuwe kwa yeyote anayekusaidia! Maana Mungu wako ndiye anayekusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakubwa katika kundi lake.