2 Samweli 16:22 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200222 Kwa hiyo, watu wakamupigia Abusaloma hema kwenye paa, naye akalala na wahabara za baba yake, watu wote wa Israeli wakiwa wanaona. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Nyuma, Daudi alifika katika nyumba yake kule Yerusalema. Mufalme aliwatwaa wahabara wake kumi ambao alikuwa amewaacha kwa kuangalia nyumba yake, akawaweka kwenye nyumba moja wapate kulindwa, akawatunza vizuri, lakini hakulala nao. Kwa hiyo wahabara hao wakakuwa wakifungwa mpaka siku za kufa kwao, wakaishi kama vile walikuwa wajane.