15 Kisha, Daudi akamwita mumoja kati ya vijana wake akamwambia: “Umwue mutu huyu!” Yule kijana alimupiga yule Mwamaleki, naye akakufa.
Halafu mufalme Solomono akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada; naye akamwendea Adonia, akamwua.
Basi, Benaya mwana wa Yehoyada akaenda katika hema, akamwua Yoabu ambaye alizikwa katika shamba lake, katika mbuga.
Hapo, mufalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada, naye akatoka, akamupiga na kumwua Simei. Basi, ufalme ukaimarika chini ya Solomono.
Anavunja mipango ya wadanganyifu, matendo yao yasipate mafanikio.
Faida mwovu anayopata ni ya uongo, lakini anayetenda mema, hakika atapata faida.
Kisha akamwambia Yeteri, muzaliwa wake wa kwanza: “Simama, uwaue.” Lakini Yeteri akaogopa kutwaa upanga wake maana alikuwa angali kijana.