Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Yawe zaidi ya toni elfu tatu za zahabu, zaidi ya toni elfu moja za feza pamoja na shaba na chuma visivyoweza kupimwa maana ni vingi sana. Nimetayarisha mbao na mawe. Lakini utaweza kuongeza.
Vilevile walipeleka vyungu, majembe, makasi na miiko iliyotumiwa kwa kuchoma ubani na vyombo vingine vyote vya shaba nyeusi vilivyotumiwa katika kazi ya hekalu,
Shaba yote nyeusi Solomono aliyotumia kwa kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na viikalio kwa ajili ya nyumba ya Yawe haikuweza kupimwa kwa uzito.
Juu ya vitu Solomono alivyotengeneza: nguzo mbili, birika kubwa moja na sanamu za ngombe dume kumi na mbili za shaba nyeusi ambazo zilikuwa chini ya hilo birika kubwa pamoja na misingi, shaba nyeusi ya vitu hivi vyote ilikuwa na uzito mwingi sana.