1 Wafalme 3:4 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20024 Wakati mumoja, Solomono alikwenda kutoa sadaka kule kwenye kilima cha Gibeoni, maana palikuwa ndipo pahali pakubwa pa ibada. Ilikuwa ni kawaida ya Solomono kutoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa katika mazabahu hiyo. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Miji ya ukoo za kabila la Benjamina ni: Yeriko, Beti-Hogla, Emeki-Kesisi, Beti-Araba, Zemaraimu, Beteli, Awimu, Para, Ofura, Kefari-Amoni, Ofuni na Geba. Jumla ya miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Gibeoni, Rama, Beroti, Misipa, Kefira, Moza, Rekemu, Iripeli, Tarala, Zela, Ha-Elefu, Yebusi, ni kusema Yerusalema, Gibea na Kiriati-Yearimu. Jumla ya miji kumi na mine pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu watu wa kabila la Benjamina na ukoo zao waliyopewa.