Nitafanya hivyo kwa sababu Solomono ameniacha, akaabudu miungu ya kigeni: Astaroti mungu wa Wasidoni, Kemosi mungu wa Wamoabu, na Milkomu mungu wa Waamoni. Solomono ameniasi, ametenda maovu mbele yangu. Hakutii masharti yangu na maagizo yangu kama Daudi baba yake alivyofanya.
Maana, alipokuwa muzee, wake zake walimupotosha hata akaitumikia miungu mingine, wala hakukuwa mwaminifu kabisa kwa Yawe, Mungu wake, kama baba yake Daudi alivyokuwa mwaminifu.
“Ee Yawe, ninakusihi ukumbuke jinsi nilivyokutumikia kwa uaminifu na kwa moyo wangu wote na kutenda mazuri mbele yako.” Hezekia akalia kwa uchungu sana.
bila kujitukuza mwenyewe juu ya wandugu zake, wala kuiweka kando amri hii kwa namna yoyote, kusudi aweze kudumu katika utawala, yeye na wazao wake katika Israeli.
Ninakuomba unisamehe mimi mujakazi wako. Yawe atakupa jamaa imara kwa sababu, wewe bwana wangu, unapigana vita ya Yawe. Wakati wote wa maisha yako usipatikane na ubaya wowote.