Naye Yawe akawatia hofu kubwa mbele ya Waisraeli ambao waliwaua watu wengi kule Gibeoni wakiwakimbia kwenye njia ya muteremuko wa Beti-Horoni mpaka Azeka na Makeda ambako vilevile waliwaua watu wengi sana.
Samweli alipokuwa anatolea ile sadaka ya kuteketezwa, Wafilistini walikaribia kuwashambulia Waisraeli. Lakini Yawe akatoa sauti kubwa ya ngurumo juu ya Wafilistini, na kuwavuruga Wafilistini, nao wakashindwa mbele ya Waisraeli.