Vilevile katika inchi ya kabila la Isakari na kabila la Aseri, kabila la Manase lilipatiwa miji ya Beti-Seani na Ibuleamu pamoja na vijiji vyake, na miji ya Dori, Eni-Dori, Tanaki na Megido pamoja na wakaaji na vijiji vyake; na sehemu moja ya tatu ya Nafati.
Watu wa kabila la Manase hawakuwafukuza wakaaji wa miji ya Beti-Seani na vijiji vyake, Tanaki na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake, Ibileamu na vijiji vyake, na Megido pamoja na vijiji vyake. Wakanana waliendelea kukaa kule.
Basi, Daudi akamwambia Ahimeleki: “Una upanga au mukuki ambao unaweza kunipatia? Kwa maana shuguli za mufalme zilinilazimisha niondoke haraka, nami niliondoka bila upanga wangu wala silaha nyingine yoyote.”
mashujaa wote waliondoka, wakasafiri usiku kucha, wakaondoa mwili wa Saulo na miili ya wana wake kutoka ukuta wa Betisani, wakakuja nayo mpaka Yabesi na kuiteketeza kwa moto kule.
Samweli akawaambia Waisraeli: “Kama munamurudilia Yawe kwa moyo wenu wote, basi mutupilie mbali miungu ya kigeni na sanamu za Astaroti. Muelekeze mioyo yenu kwa Yawe, na kumutumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka katika mikono ya Wafilistini.”