Halafu Waamaleki na Wakanana, waliokuwa wakiishi katika inchi hiyo ya milima, wakashuka, wakawashambulia na kuwashinda. Wakawafukuza mpaka muji wa Horma.
Yawe akasikia ombi lao, akawapa ushindi juu ya Wakanana. Waisraeli wakaangamiza kabisa Wakanana pamoja na miji yao. Kwa hiyo pahali pale pakaitwa Horma, ni kusema “Maangamizi”.
Watu wa kabila la Yuda walishirikiana na wandugu zao, watu wa kabila la Simeoni, wakawashinda Wakanana waliokaa Sefati. Wakaangamiza kabisa muji ule na kugeuza jina lake kuwa Horma, ni kusema “Maangamizo”.