1 Samweli 30:10 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
10 Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile kundi akiwa na watu mia ine. Watu mia mbili wakabaki pale kwa sababu walichoka sana hata hawakuweza kuvuka kijito kile.
Hivyo, Saulo na watu wake wakajipanga na kuingia katika vita na Wafilistini. Lakini Wafilistini walianza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kwa muvurugiko mukubwa.
Daudi akawarudilia wale watu mia mbili ambao waliachwa kwenye kijito cha Besori kwa sababu walikuwa wamechoka kwa kumufuata. Wale watu walipomwona Daudi pamoja na wale waliokuwa pamoja naye, wakaenda kumupokea. Daudi alipofika karibu na watu hao, akawasalimia.
Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu mia sita aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta wamoja kati ya watu waliotekwa wameachwa pale.