Yawe akamwita tena: “Samweli!” Samweli akaamuka, akamwendea Eli na kumwambia: “Nimekuja, maana umeniita.” Lakini Eli akamwambia: “Sikukuita mwana wangu, ulale tena.”
Yawe akamwita Samweli kwa mara ya tatu. Samweli akaamuka, akamwendea Eli na kumwambia: “Nimekuja, maana umeniita.” Halafu Eli alitambua kwamba Yawe ndiye aliyemwita Samweli.