Sarai akamwambia Abramu: “Lazima ya ubaya ninaotendewa ikuwe juu yako. Mimi nilikupa mujakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa kitu bure mbele ya macho yake! Yawe ahukumu kati yako na mimi!”
Daudi akatoka inje kwa kuwapokea, akawaambia: “Ikiwa mumekuja kwangu kama warafiki kwa kunisaidia basi ninawapokea kwa moyo wote, lakini kama mumekuja kwa kunitoa kwa waadui zangu, ingawa sijatenda ovu lolote, Mungu wa babu zetu awaone na kuwaazibu ninyi.”
Angalia kama vile leo maisha yako yalivyokuwa na bei kali mbele yangu, ndivyo maisha yangu yapate kuwa na bei kali mbele ya Yawe; naye aniokoe kutoka taabu zote.”