Mimi nitakuja na kusimama karibu na baba yangu kule katika shamba pahali utakapokuwa. Pale nitaongea naye juu yako, na kitu chochote nitakachogundua kutoka kwake, nitakuelezea.”
Halafu Yonatani akamwambia Daudi: “Uende na amani. Tumekwisha wote kuapa kwa jina la Yawe kwamba Yawe akuwe mushuhuda kati yetu milele, na kati ya wazao wangu na wazao wako milele.”
Hivyo unitendee mema maana umefanya agano nami, mimi mutumishi wako, mbele ya Yawe. Lakini, kama nimefanya kosa basi, uniue wewe mwenyewe. Kwa nini unipeleke kwa baba yako kusudi aniue?”