Yule kijana alipokwisha kuondoka, Daudi akasimama na kutoka pahali alipojificha karibu na lundo la mawe. Aliinama chini kwa heshima mara tatu mbele ya Yonatani. Wote wawili, Daudi na Yonatani, wakakumbatiana na kulia. Daudi alikuwa na uchungu zaidi kuliko Yonatani.