Sarai akamwambia Abramu: “Lazima ya ubaya ninaotendewa ikuwe juu yako. Mimi nilikupa mujakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa kitu bure mbele ya macho yake! Yawe ahukumu kati yako na mimi!”
Halafu Yonatani akamwambia Daudi: “Uende na amani. Tumekwisha wote kuapa kwa jina la Yawe kwamba Yawe akuwe mushuhuda kati yetu milele, na kati ya wazao wangu na wazao wako milele.”