Lakini Eleazari alisimama imara na kupigana na Wafilistini mpaka mukono wake uliposhindwa kupindika, ukabaki umebania upanga wake. Siku hiyo, Yawe alijipatia ushindi mukubwa. Nyuma ya ushindi ule, Waisraeli walirudi pahali Eleazari alipokuwa na kuteka vitu kutoka kwa Wafilistini waliouawa.
Lakini wote wanaokuangamiza, wataangamizwa vilevile, na waadui zako wote watapelekwa katika uhamisho; nao wanaokukamata mateka watakamatwa mateka, nao wanaokuwinda, nitawawinda.
Halafu watu wa Israeli na watu wa Yuda walianza kupiga kelele za ushindi, wakawafuatilia Wafilistini mpaka Gati, kwenye milango ya muji wa Ekroni, hata Wafilistini walioumizwa katika vita walikufa katika njia tangu Saraimu mpaka Gati na Ekroni.
Alipomwua yule Mufilistini Goliati, alihatarisha maisha yake, naye Yawe aliwapa Waisraeli ushindi mukubwa. Wewe ulipoona jambo lile ulifurahi. Kwa nini unataka kutenda zambi kwa kumwanga damu isiyokuwa na kosa kwa kumwua Daudi bila sababu?”