Yawe ambaye ameniokoa toka katika makucha ya simba na dubu, ataniokoa kutoka kwa Mufilistini huyu.” Saulo akamwambia: “Kwenda, naye Yawe akuwe pamoja nawe.”
Daudi akajifunga upanga wa Saulo, akajaribu kutembea; lakini akashindwa kwa sababu hakuzoea nguo kama hizo. Akamwambia Saulo: “Siwezi kwenda katika vita nikiwa nimevaa nguo hizi, maana mimi sijazizoea.” Kwa hiyo, akazivua.