1 Samweli 14:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20026 Yonatani akamwambia yule kijana aliyemubebea silaha: “Kuja, tuende kwenye ile kambi ya hawa watu wasiotahiriwa. Labda Yawe atatusaidia, maana Yawe haokoi kwa kutegemea wingi au uchache wa watu.” အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Hapo Asa akamulilia Yawe, Mungu wake, akisema: “Ee Yawe, hakuna mwingine kama wewe, mwenye uwezo wa kusaidia jeshi likuwe zaifu au lenye nguvu. Utusaidie, ee Yawe, Mungu wetu, kwa sababu sisi tunakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja kupigana vita na jeshi hili kubwa ajabu. Ee Yawe, wewe ndiwe Mungu wetu; usimuruhusu mwanadamu yeyote ashindane nawe.”