Daudi alipomwomba Yawe shauri, Yawe alimwambia: “Usiwashambulie kutoka hapa unapokuwa, lakini zunguka nyuma yao na kuwashambulia kutokea mbele ya miti ya miforosadi.
Waisraeli wakaenda Beteli kuomba shauri kwa Mungu, wapate kujua kabila ambalo litakwenda kwanza kupigana na watu wa kabila la Benjamina. Yawe akataja kabila la Yuda liende kwanza.
Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa Haruni alikuwa na kazi ya kutumika mbele yake. Waisraeli wakamwuliza Yawe: “Twende tena kupigana na wandugu zetu, watu wa kabila la Benjamina?” Yawe akawaambia: “Muende. Kesho nitawatia katika mikono yenu.”