Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




1 Samweli 1:17 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

17 Halafu Eli akamwambia: “Kwenda kwa amani; naye Mungu wa Israeli akupe kile ulichomwomba.”

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




1 Samweli 1:17
14 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Yawe. Naye Yawe akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba.


Mufalme akamwambia: “Basi, kwenda kwa amani.” Abusaloma akaondoka kwenda Hebroni.


Elisha akamwambia: “Kwenda kwa amani.” Namani akaenda zake. Alipokuwa bado hajafika mbali,


Lakini Yebesi alimwomba Mungu wa Israeli akisema: “Ee Mungu, ninakusihi unibariki na kupanua mipaka yangu. Mukono wako ukuwe pamoja nami na unilinde kutokana na jambo lolote ovu, na mateso yasinipate.” Naye Mungu akamupa yale aliyoomba.


Yesu akamwambia: “Binti yangu, imani yako imekuponyesha. Ujiendee na amani, ugonjwa wako umepona!”


Lakini Yesu akamwambia tena yule mwanamuke: “Kwenda na amani, imani yako imekuokoa.”


Na Yesu akamwambia: “Binti yangu, imani yako imekuponyesha. Ujiendee na amani.”


Yule kuhani akawaambia: “Muende kwa amani. Yawe anaichunga safari yenu.”


Usinizanie kuwa mimi ni mwanamuke asiyefaa kitu. Kwa muda wote huu nimekuwa nikisema mahangaiko yangu na taabu yangu.”


Mume wake Elekana, akamujibu: “Fanya unaloona linafaa. Ngojea mpaka utakapomwachisha mutoto kunyonya. Yawe afanye kiapo chako kuwa kweli.” Basi, Hana alibaki kwake, akaendelea kumulea mutoto wake mpaka alipomwachisha kunyonya.


Halafu Yonatani akamwambia Daudi: “Uende na amani. Tumekwisha wote kuapa kwa jina la Yawe kwamba Yawe akuwe mushuhuda kati yetu milele, na kati ya wazao wangu na wazao wako milele.”


Kisha, Daudi akapokea vitu vyote ambavyo Abigaili alikuwa amemuletea, akamwambia Abigaili: “Rudi kwako na amani. Mimi nimeyasikia uliyosema, na ombi lako nimelipokea.”


Hivyo sasa, urudi kwa nyumba. Kwenda kwa amani kusudi usiwachukize wakubwa wa Wafilistini.”


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ