Yawe wa majeshi atawalinda watu wake, nao watawaangamiza waadui zao. Watapiga kelele katika vita kama walevi, wataimwanga damu ya waadui zao. Itatiririka kama damu ya nyama wanaotolewa kwa sadaka iliyomiminwa juu ya mazabahu kutoka ndani ya bakuli.
Na ni hivi vilevile Roho wa Mungu anatusaidia katika uzaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba sawa inavyopaswa. Lakini Roho wa Mungu yeye mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa kuugua kusikoweza kuelezwa.