11 Lakini sasa sitawatendea hao watu wa taifa hili wanaobaki kama vile zamani. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.–
Siku hiyo mutasema: Ninakushukuru, ee Yawe, maana ingawa ulinikasirikia, hasira yako imetoweka, nawe umenifariji.
Ingawa sasa hakuna ngano ndani ya gala, nayo mizabibu, tini, mikomamanga na mizeituni haijazaa kitu, lakini tangu leo, nitawabariki.
Hatukaripii siku zote, wala hasira yake haidumu milele.
Wivu wa Efuraimu juu ya Yuda utakoma, hakutakuwa tena uadui kati ya Yuda na Efuraimu.
Lakini sasa mufikiri vizuri juu ya mambo yatakayotukia. Mbele ya kuanza kujenga upya nyumba yangu,