Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na maeneo ya kandokando ya Yerusalema, kutoka inchi ya kabila la Benjamina, kutoka Shefela, kutoka inchi ya milima na kutoka Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka zingine za kawaida, sadaka ya mavuno na ya ubani wenye harufu nzuri pamoja na matoleo ya shukrani. Hivyo vyote watavileta katika nyumba ya Yawe.