Nilipoangalia, niliona wanawake wawili wanatokea; walikuwa wakirushwa na upepo, nao walikuwa na mabawa yenye nguvu kama ya korongo. Wanawake wale wakakiinua kile kikapu katika anga.
Nami nikamwuliza yule malaika aliyezungumuza nami: Pembe hizi zina maana gani? Yeye akanijibu: Pembe hizi zina maana ya yale mataifa ambayo yaliwatawanya watu wa Yuda, Israeli na Yerusalema.