Silaha zote zilizotengenezwa kwa kukuzuru wewe hazitafaa kwa kitu chochote. Mutu akikushitaki, utamushinda. Hiyo ndiyo haki niliyowapangia watumishi wangu. Hizo ndizo haki nilizowahakikishia. –Ni ujumbe wa Yawe.
Nitaufanya Yerusalema kuwa kama kikombe cha divai; na mataifa yanayokuwa kandokando yake yatakunywa na kuyumbayumba kama walevi. Muji Yerusalema utakaposhambuliwa, hata miji yote ya Yuda itashambuliwa.
Halafu, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalema, wote wanaoshambulia ukuta wake na kuutia wasiwasi, watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku.