Yoshua 21:6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
6 Watu wa ukoo wa Gersoni wakapewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Aseri, Nafutali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase kule Basani.
Jamaa za Merari zilizobakia, zilipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho kandokando ya miji hiyo. Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na mashamba yake ya malisho na Tabori pamoja na mashamba yake ya malisho.
Jamaa za ukoo wa Gersoni walipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho: katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Basani pamoja na mashamba yake ya malisho, Astaroti pamoja na mashamba yake ya malisho.