Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Yoeli 2:5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

5 Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima, wananguruma kama magari yenye kukokotwa na farasi, wanavuma kama moto wa majani yenye kukauka. Wamejipanga kama kundi kubwa la waaskari tayari kabisa kufanya vita.

Gade chapit la Kopi




Yoeli 2:5
9 Referans Kwoze  

Na juu ya vifua vyao kulikuwa vitu vinavyofanana na ngao za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama uvumi wa magari yanayovutwa na farasi wengi wanaokimbia mbio kwenda kwa vita.


Kwa hiyo, kama vile moto unavyoteketeza nyasi, kama vile majani yanavyotoweka ndani ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza, na maua yao yatakavyopeperushwa juu kama mavumbi. Maana wameacha sheria ya Yawe wa majeshi, wamezarau neno la yule Mutakatifu wa Israeli.


Yawe atawafanya watu wote waisikie sauti yake tukufu na pigo la nguvu yake lionekane kwa hasira nyingi. Kutakuwa ndimi za moto mukali, ngurumo, zoruba na mvua ya mawe.


Yeye anashika lungo katika mikono yake kwa kupepeta ngano. Atakusanya ngano na kuitia katika gala yake, lakini atateketeza maganda katika moto usiozimika.”


Ni wewe unayemufanya farasi aruke kama nzige? Mulio wake wa maringo ni wa ajabu!


Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakali wasiokuwa na huruma. Vishindo vyao ni kama uvumi wa bahari, wamepanda juu ya farasi. Wamejipanga tayari kwa vita na wewe Babeli!


Basi, watu wote wakatawanyika kila pahali katika inchi ya Misri wakitafuta nyasi za kutengeneza matofali.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite