Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Yoane 21:1 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

1 Nyuma ya mambo hayo, Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kandokando ya ziwa la Tiberia. Angalia sasa namna alivyowatokea:

Gade chapit la Kopi




Yoane 21:1
11 Referans Kwoze  

Nyuma ya maneno hayo, Yesu akavuka ziwa la Galilaya (linaloitwa vilevile Tiberia).


Na vilevile vyombo vingine vilivyotoka katika muji Tiberia vilifika karibu na pahali pale walipokula mikate, Bwana alipokuwa amekwisha kushukuru Mungu.


Halafu wale wanafunzi kumi na mumoja wakaenda Galilaya kwa mulima ule Yesu aliowaagiza.


Muende upesi kuwaambia wanafunzi wake kwamba amefufuka, naye anawatangulia Galilaya, ni kule watakapomwona. Basi, nimekwisha kuwaambia ninyi.”


Lakini nitakapokwisha kufufuka, nitawatangulia Galilaya.”


Hii ndiyo mara ya tatu Yesu aliyowatokea wanafunzi wake tangu alipofufuka.


Kisha, Yesu akawatokea wanafunzi wawili, akiwa na sura ingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda kwenye vijiji.


Muende sasa kupasha habari kwa wanafunzi wake na kwa Petro, muwaambie kwamba anawatangulia Galilaya; nao watamwona kule sawa vile alivyowaambia.”


Kwa mwisho Yesu akawatokea wanafunzi kumi na mumoja walipokuwa wakikula. Naye akawakaripia kwa sababu ya kutokuamini kwao na kwa sababu ya ugumu wao. Kwa maana hawakusadikia wale waliomwona nyuma ya kufufuka kwake.


Nyuma ya kufa kwake, alijionyesha kwao kwa namna nyingi kwa kuhakikisha kwamba amefufuka. Kwa muda wa siku makumi ine, alionekana kwao na kusema nao juu ya maneno yanayoelekea Ufalme wa Mungu.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite