Sisemi hivi kwa kuwaamuru, lakini kwa njia ya kuwaelezea habari za bidii ya wengine, ninataka kuwapima kusudi upendo wenu upate kutambulikana kuwa wa kweli.
Yesu akawaita wanafunzi wake, na kuwaambia: “Ninawasikilia watu hawa huruma, kwa sababu wamekaa nami sasa kwa muda wa siku tatu, nao hawana chakula tena. Nami sitaki kuagana nao pasipo kula, kusudi wasiregee katika njia.”