Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Walawi 7:7 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

7 Sheria ni moja kuelekea sadaka kwa ajili ya kosa na sadaka kwa ajili ya zambi. Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeitwaa.

Gade chapit la Kopi




Walawi 7:7
11 Referans Kwoze  

Munajua hakika kuwa wale wanaotumika katika hekalu wanapata chakula chao ndani ya hekalu. Na wale wanaotumika kwa kutoa sadaka juu ya mazabahu wanapata sehemu yao kutoka sadaka zile.


Kisha atachinja yule mwana-kondoo katika Pahali Patakatifu, wanapochinjia nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi na sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka hii kwa ajili ya kosa na vilevile sadaka kwa ajili ya zambi, ni mali ya kuhani. Ni sadaka takatifu kabisa.


Muangalie mufano wa Waisraeli: wale wanaokula vitu vinavyotolewa sadaka juu ya mazabahu wanaungana na Mungu kwa njia ya sadaka ile.


Yawe akamwambia Musa:


Kuhani anayetolea sadaka ya kuteketezwa ya mutu yeyote, atatwaa ngozi ya nyama aliyetolewa.


Wafanyakazi waliosimamia kazi hii walikuwa waaminifu kabisa. Kwa hiyo hakukuwa lazima ya kuwaomba watoe hesabu ya matumizi ya feza.


Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.


Sehemu inayobaki ya sadaka ya ngano, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Yawe kwa moto.


Lakini ikiwa mutu huyo amekufa na hana ndugu wa karibu ambaye anaweza kupokea malipo hayo, basi, malipo ya kosa yatatolewa kwa Yawe kwa ajili ya makuhani; malipo haya ni pamoja na kondoo dume wa upatanisho ambaye atatumiwa kwa kumufanyia upatanisho kwa ajili ya zambi yake.


Feza zilizotolewa kwa sadaka za malipo kwa ajili ya kosa na kwa sadaka za usamehe wa zambi hazikuingizwa katika nyumba ya Yawe. Hizo zilikuwa ni mali ya makuhani.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite