Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Walawi 6:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

9 Unga uliobakia Haruni na wazao wake makuhani wataukula bila kutiwa chachu. Wataukula kwenye Pahali Patakatifu katika kiwanja cha hema la mukutano.

Gade chapit la Kopi




Walawi 6:9
10 Referans Kwoze  

Uwaambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa hii: wana-kondoo wawili wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema chochote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.


Siku ya Sabato, mutatoa sadaka ya wana-kondoo dume wawili wa mwaka mumoja wasiokuwa na kilema, sadaka ya vyakula ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta, na sadaka yake ya kinywaji.


Mumoja wa makuhani atatwaa mukono mumoja wa unga wa sadaka ya vyakula pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya mazabahu kama vile sehemu ya ukumbusho. Harufu yake itamupendeza Yawe.


Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.


Sehemu inayobaki ya sadaka ya ngano, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Yawe kwa moto.


Kuhani anayetolea sadaka hiyo ndiye atakayeikula. Itakuliwa katika Pahali Patakatifu, kwenye kiwanja cha hema la mukutano.


Haruni na wazao wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo maana ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Yawe kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite