Bwana wetu Yawe atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuondoa haya ya watu wake katika dunia yote. Yawe amesema hivyo.
Kwa maana Mwana-Kondoo anayekuwa katikati ya kiti cha kifalme, atawachunga na kuwaongoza kwenye chemichemi ya maji ya uzima. Naye Mungu atawapanguza machozi yao yote.”
Mwangaza wako muchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Yawe ni mwangaza wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.
Waliokombolewa na Yawe watarudi, watakuja Sayuni wakipiga vigelegele. Watakuwa wenye furaha ya milele, watajaliwa furaha na shangwe; huzuni na kilio vitatoweka kabisa.
Watu wako uliowakomboa, ee Yawe, watarudia, watakuja Sayuni wakiimba; watajaa furaha ya milele, watapata furaha na shangwe. Huzuni na maombolezo vitatoweka kabisa.
Halafu wabinti zao watafurahi na kucheza, vijana na wazee watashangilia kwa furaha. Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, nitawafariji na kuwapa furaha pahali pa huzuni.
Enyi watu wa Sayuni, enyi watu wa Yerusalema, hakika ninyi hamutaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikia.
na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.
Hakutakuwa tena kitu chochote kinacholaaniwa na Mungu. Kiti cha kifalme cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwa ndani ya muji ule, na watumishi wa Mungu watamwabudu.
Siku Bwana atakaporudi, itatimia kama vile mwizi anavyokuja. Siku ile mbingu zitatoweka kwa shindo kubwa, na viumbe vyote vinavyoangaza katika mbingu vitayeyuka. Dunia na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake vitateketezwa.
Inanipasa kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifo! Ewe kifo, mapigo yako ni wapi? Ewe kuzimu, kuangamiza kwako ni wapi? Mimi sitawaonea tena huruma!
Watakuja na kuimba kwa sauti juu ya mulima Sayuni, watapata utukufu juu ya wema wangu mimi Yawe, kwa ajili ya ngano, divai na mafuta ninavyowapa, kwa ajili ya kondoo na ngombe vilevile; maisha yao yatakuwa kama bustani iliyotiliwa maji, wala hawataregea tena.
Bahari ikawarudisha wafu waliozama ndani yake. Kifo na kuzimu zikarudisha wafu waliokuwa ndani yao. Na kila mumoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.