Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Ufunuo 10:9 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

9 Nami nikaenda karibu na yule malaika, nikamwomba anipe kile kitabu kidogo. Naye akaniambia: “Ukitwae na ukikule, kitakuwa uchungu katika tumbo lako, lakini kitakuwa kitamu kama asali ndani ya kinywa chako.”

Gade chapit la Kopi




Ufunuo 10:9
7 Referans Kwoze  

Palepale maneno yako yaliponifikia, niliyameza; nayo yakanifurahisha, yakakuwa matamu katika moyo wangu, maana mimi ninajulikana kwa jina lako, ee Yawe wa majeshi.


Lakini, ewe mwanadamu, usikilize ninayokuambia, wala usikuwe mwasi kama watu hao waasi. Ufungue kinywa chako, ukule ninachokupa.


Basi, Roho akaninyanyua juu na kunipeleka mbali. Yawe alinijaza uwezo wake. Nami nikaenda nikiwa na uchungu na hasira katika roho yangu.


Sijaacha hata kidogo kushika amri yake; maneno yake nimeyatunza ndani ya moyo wangu.


Kwa sababu ya makosa haya, kasirani ya Mungu itawaangukia wale wanaomwasi.


Basi nikatwaa kitabu kile kidogo toka katika mukono wake, nikakikula. Kikakuwa kitamu kama asali ndani ya kinywa changu, lakini wakati nilipokimeza, nikasikia uchungu ndani ya tumbo langu.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite