Boazi alipomaliza kula na kunywa, akachangamuka. Akakwenda karibu na lundo la shayiri, akalala. Ruta akakwenda polepole akafunua miguu yake na kulala pale.
Akauliza: “Wewe ni nani?” Ruta akajibu: “Ni mimi Ruta, mujakazi wako. Kwa sababu wewe ni wa jamaa yangu wa karibu, uitande nguo yako juu ya mujakazi wako.”