6 Kwa hiyo, Ruta akakwenda kule katika kiwanja cha kupepetea, akafanya jinsi mama mukwe wake alivyomwamuru.
Mwana wangu, sikiliza mafundisho ya baba yako, wala usizarau mashauri ya mama yako;
Halafu mama yake akawaambia watumishi: “Mufanye kila kitu atakachowaambia.”
Uwaheshimu baba yako na mama yako, kusudi uishi maisha marefu katika inchi ninayokupatia mimi Yawe, Mungu wako.
Ninyi ni warafiki zangu, kama mukifanya sawa ninavyowaagiza.
Ruta akajibu: “Nitafanya yote uliyoniambia.”
Boazi alipomaliza kula na kunywa, akachangamuka. Akakwenda karibu na lundo la shayiri, akalala. Ruta akakwenda polepole akafunua miguu yake na kulala pale.
Esteri alikuwa hajatambulisha ukoo wala kabila lake, maana Mordekayi alikuwa amemwonya asifanye hivyo.