Biblia Todo Logo
Bib sou entènèt

- Piblisite -




Ruta 2:2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

2 Siku moja, Ruta wa Moabu akamwambia Naomi: “Muniruhusu niende kukusanya masalio ya mavuno pahali nitakapopata kukubaliwa na mwenye shamba.” Naomi akamwambia: “Basi, uende binti yangu.”

Gade chapit la Kopi




Ruta 2:2
9 Referans Kwoze  

Unapovuna mavuno yako katika shamba, usivune kabisa mpaka kwenye mupaka wa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. Utawaachia hayo wamasikini na wageni. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.


Utakapovuna mavuno ya inchi yako, usivune kabisa mpaka kwenye mupaka wa shamba wala usirudi nyuma kukusanya mabaki.


Aliniomba nimuruhusu awafuate nyuma wavunaji naye akiokota masalio kati ya miganda. Basi alikuja na amefanya kazi tangu asubui na ni sasa tu amekwenda kupumzika katika kibanda.”


Usipitepite hata kidogo ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usitie maisha ya mwenzako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ni Yawe.


Musirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Utawaachia wamasikini na wageni. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.


Basi Ruta akaenda katika shamba, akawafuata wavunaji naye akiyaokota masuke waliyoyaacha. Na kumbe akajikuta katika shamba la Boazi, yule wa ukoo wa Elimeleki.


Nina ngombe, punda, makundi ya kondoo, watumwa na wajakazi. Ninakutumia ujumbe huu, bwana wangu, kusudi nipate kukubaliwa mbele yako.’ ”


Hana akasema: “Ninaomba nami mujakazi wako nipate kukubaliwa mbele yako.” Hana akaenda zake, akakula chakula na hakukuwa na huzuni tena.


Swiv nou:

Piblisite


Piblisite