Tena imeandikwa kwamba: “Jiwe lile ni la kukwalisha watu, nalo ni la kuwaangusha.” Wamejikwaa kwa sababu hawakuamini neno la Mungu, na hivi ndivyo walivyopanga kwa ajili yao tangu mwanzo.
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nami nitawaongoza nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyooka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efuraimu ni muzaliwa wangu wa kwanza.