23 Halafu utaweza kwenda zako kwa usalama, wala muguu wako hautajikwaa.
Anayeishi kwa ukamilifu anaishi salama, lakini anayepotosha maisha yake atagunduliwa.
Ukitembea hatua zako hazitazuizwa, wala ukikimbia hautajikwaa.
Hatakuacha uanguke; mulinzi wako hasinzii.
Sheria ya Mungu wake ni ndani ya moyo wake, naye hapiti pembeni katika mwenendo wake.
Mimi nitawaimarisha watu wangu, nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza. Ni mimi Yawe ninayesema hivyo.
Analinda mienendo ya watu wanaofuata sheria yake, na kuchunga njia za waaminifu wake.
Yawe atakulinda katika shuguli zako zote tangu sasa na hata milele.
Wanaopenda sheria yako wana amani kubwa; hakuna kinachoweza kuwaangusha.
Yatakuongoza katika njia yako, yatakulinda wakati unapolala, yatakushauria unapoamuka.
Hawachoki wala hawajikwai; hawasinzii wala hawalali; hakuna mukaba wao uliofunguka wala kamba ya kiatu iliyokatika.
Aliwaongoza katikati ya vilindi vya bahari, wakapita humo kama farasi bila kujikwaa.